Dodoma. Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani, Hamad Yusufu amejibu upya swali
lililomponza bosi wake wa zamani, Charles
Kitwanga.
Uamuzi wa kurudia swali hilo ulitolewa juzi
na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisema
swali hilo lilijibiwa katika hali ya ulevi na
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na
wabunge wakaomba mwongozo kuhusu
majibu yaliyotolewa.
Kitwanga aliondolewa katika nafasi yake na
Rais John Magufuli baada ya kujibu ya swali
hilo akiwa amelewa.
Leo, Masauni amejibu swali hilo namba 211
la Mbunge wa Viti Maalumu Devota Minja
(Chadema) na kuonyesha utofauti mkubwa
kati ya majibu yake na yale yaliyotolewa
mwishoni mwa wiki na aliyekuwa Waziri
wake.
Swali hilo ambalo awali lilikuwa namba 205,
liliulizwa na Devota Minja akitaka kujua
Serikali ina mpango gani wa kuboresha
makazi ya polisi na askari magereza
wanaoishi katika nyumba chakavu
zisizokuwa na hadhi ukilinganisha na kazi
zao kwa jamii.
Nyakati zote hizo, swali hilo limeulizwa na
wabunge tofauti wa Chadema kutokana na
Minja kutokuwapo, mara ya kwanza
likiulizwa na Suzan Kiwanga (Mlimba) na
leo Joseph Selasini wa Jimbo la Rombo.
Tofauti ya majibu ya Kitwanga, Masauni
ametoa takwimu katika ujenzi wa nyumba
9,500 za Magereza nchi nzima, lakini kwa
upande wa nyumba za Polisi majibu
yalikuwa yaleyale.
Jumatano, 25 Mei 2016
Ulipata majibu sahihi ya swali lililo mponza kitwanga? Kama hukubahatika kuyapata haya hapa kwa ajili yako
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni