Jumanne, 24 Mei 2016

Uliipata hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni ? Usijali haijakupita hii hapa

HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI
BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA
FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)
AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA
KAMBI RASMI YA UPINZANI
BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA
MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA
MWAKA WA FEDHA 2016/17.
Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge,
Toleo la Januari, 2016
_________________________________
1. SHERIA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA
MAWAZIRI (MINISTERS – DISCHARGE OF
MINISTERIAL FUNCTIONS – ACT, 1980.
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 5(1) kinaweka
masharti kwa Rais kutengeneza mwongozo wa
muundo na utekelezaji wa majukumu ya Serikali
yake.
Inasomeka ifuatavyo: Nanukuu “the President
shall from time to time by notice published in
the Gazette, specify the departments, business
and other matters and responsibility for which
he has retained for himself or he has assigned
under his direction to any minister and may in
that notice specify the effective date of the
assumption of that responsibility…….” mwisho
wa kunukuu.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali inafanya
kazi bila kuwa na mwongozo wa utendaji wake
na kazi kwa wizara mbalimbali. Hii ina maana
kwamba Serikali inafanya kazi kwa kauli za Rais
na Mawaziri bila kufuata mwongozo wowote
wenye msingi na uhalali wa kisheria.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa mwongozo wa
utendaji wa Serikali kwa kila Wizara
(Instrument) unaotumika ni ule uliochapishwa
kwenye gazeti la Serikali namba 494A la tarehe
17/12/2010. Kwa mujibu wa Instrument hiyo,
majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni:
 Coordination of Government Business
 Leader of Government Business in the National
Assembly
 Link between Political Parties and Government.
 National Festivals and Celebration of
Management of Civic Contingencies (relief).
 Facilitation and Implementation of Plans for the
Development of Dodoma as Capital of Tanzania.
 Coordination and Supervision of Transfer of
the Government to Dodoma.
 Government Press Services.
 Investment, Economic Empowerment, Public-
Private-Partnership (PPP), Poverty alleviation
Policies and their Implementation.
 Facilitation of the Development of Informal
Sector.
 Performance Improvement and Development of
Human Resources under this Office
 Extra – Ministerial Department, Parastatal
Organisations, Agencies, Programmes and
Projects under this Office.
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL
GOVERNMENT:
 Decentralization by Devolution (D by D), Rural
Development, Urban Development Policies and
their Implementation.
 Regional Administration.
 Primary and Secondary Education
Administration
 Dar Rapid Transit – DART.
 Performance Improvement and Development of
Human Resources under this Office.
 Extra-Ministerial Departments, Parastatal
Organisations, Agencies, Programmes and
Projects under this Office.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali hii
kuendesha kazi zake kwa Mwongozo wa 2010
ina maanisha kwamba majukumu ya Ofisi ya
Waziri Mkuu bado ni yale yale yaliyochapishwa
mwaka 2010, kwa sababu gazeti hilo la Serikali
halijafutwa.
2. UVUNJWAJI WA KATIBA NA SHERIA ZA NCHI
KUHUSIANA NA BAJETI UNAOFANYWA NA
SERIKALI
Mheshimiwa Spika, hili ni Bunge la Bajeti ambalo
kwa mujibu wa ibara ya 63(3)(b) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepewa
mamlaka ya kujadili utekelezaji wa kila Wizara
wakati wa Mkutano wa Bunge wa kila mwaaka
wa Bajeti kwa madhumuni ya kujadili na
kuidhinisha Bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, Ikiwa fedha zilizoidhinishwa
na Bunge hazikutosha kutekeleza majukumu ya
Serikali , kifungu cha 41(1) cha Sheria ya Bajeti
ya Mwaka 2015 kinaelekeza kwamba: “ Serikali
itawasilisha Bungeni kwa idhini, bajeti ya
nyongeza ya fedha zilizotumika ambazo
zimezidi kiwango kilichoidhinishwa na Bunge au
kwa madhumuni ya kugharamia mahitaji
ambayo hayakupangwa”.
Mheshimiwa Spika utaratibu huu unatiliwa
nguvu na Sheria ya Fedha za Umma wa mwaka
2001( Public Finacne Act, 2001)ambapo kifungu
cha 18 (3) na (4) kinaitaka Serikali kuleta
Bungeni bajeti ya nyongeza ( mini-budget) kwa
ajili ya kupata idhini ya Bunge ikiwa fedha
zilizoidhinishwa awali hazikutosha.
Mheshimiwa Spika, utaratibu huo wa kisheria
umekuwa ukivunjwa na Serikali kwa kufanya
matumizi ya fedha ambazo hazikuidhinishwa na
Bunge jambo ambalo linaua dhana ya madaraka
ya Bunge ya kuisimamia na kuishauri Serikali.
Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha jambo hilo,
kwa mfano bajeti ya maendeleo iliyokuwa
imeidhinishwa na Bunge kwa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha
2015/16 ilikuwa ni shilingi bilioni 883.8 ambapo
kati ya fedha hizo, fedha za ndani zilikuwa ni
shilingi bilioni 191.6
Mheshimiwa Spika, Jambo la kushangaza ni
kwamba hadi kufikia mwezi Machi 2016 Wizara
ilikuwa imeshapokea kutoka hazina shilingi
bilioni 607.4 ikiwa ni fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika, ukitazama takwimu hizo
utaona kuwa kuna ongezeko la fedha
zilizotolewa na hazina hadi kufikia mwezi
Machi 2016 ukilinganisha na fedha
zilizoidhinishwa na Bunge. Tangu kuidhinishwa
kwa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, hakuna bajeti ya
nyongeza iliyoletwa Bungeni na Serikali kwa ajili
ya kupata idhini kutokana na matakwa ya Sheria
ya Bajeti ya 2015 au sheria ya Fedha ya 2015.
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Serikali kuamua
kufanya re-allocation ya bajeti bila kupata idhini
ya Bunge ni dharau kwa bunge lakini mbaya
zaidi ni uvunjaji wa Katiba na Sheria.
3. UHURU NA MADARAKA YA MHIMILI WA
BUNGE
Mheshimiwa Spika, Ibara ya 63 (2) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalitaja
Bunge kuwa ndicho chombo kikuu katika
Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na
madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia
na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano
na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa
majukumu yake. Katika hali isiyo ya kawaida,
kifungu hiki cha Katiba kimevunjwa na badala
yake Serikali imelipoka bunge madaraka yake
na Bunge kwa maana ya uongozi wake
wanaonekana kushiriki na kukubali kupokwa
huku kwa madaraka na uhuru wake.
Mheshimiwa Spika, Bunge ni chombo cha
uwakilishi wa wananchi, na wananchi wana haki
ya kujua Bunge lao linavyofanya kazi ili wawe
na uwezo wa kuwawajibisha wawakilishi wao
iwapo hawafanyi kazi inavyostahili.
Katika hali isiyo ya kawaida, Serikali na uongozi
wa Bunge, imewapoka wananchi haki yao ya
kupata habari za Bunge kwa kuzuia mijadala
Bungeni kurushwa moja kwa moja na
televisheni ya Taifa na vyombo vingine vya
habari vya kujitegemea.
Mheshimiwa Spika, Jambo hili pia ni uvunjwaji
wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, ambayo inasema
kwamba kila mtu anao uhuru wa kuwa na
maoni na kueleza fikra zake; anayo haki ya
kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali
mipaka ya nchi; anao uhuru wa kufanya
mawasiliano na haki ya kutoingiliwa katika
mawasiliano yake na anayo haki ya kupewa
taarifa wakati wowote kuhusu matukio
mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za
wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa
jamii.
Mheshimiwa Spika, katika Mazingira kama hayo,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiko tayari
kuendelea kushiriki uvunjaji wa Katiba Sheria
na haki za msingi za wananchi.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani
haitakuwa tayari kuwasilisha hotuba yake
katika mazingira haya na inaushauri uongozi wa
Bunge kupata ufumbuzi wa haraka wa kadhia
hii ili kurejesha heshima ya Bunge na haki za
msingi za wananchi. Hivyo basi Kambi bado
inatafakari kwa kina na makini hatua za
kufuata.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA
UPINZANI BUNGENI
KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU
22 Aprili, 2016.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni