Katika siku mbili za kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyoomba kutengewa kiasi cha Sh. 135,797,787,000 katika hotuba iliyowasilishwa na Waziri wake Jumanne Maghembe, Wabunge walipata nafasi pia ya kuchangia ambapo hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega …
>>’Wakati mwingine hata mimi nashawishika kufikiria kwamba kabla hatujaingia kwenye jengo hili tuwe tunapimwa kama tumevuta marijuana, katika hali ya kawaida kijana hata kama umepigiwa kura na kuaminiwa na wananchi ukaenda kutukana lazima utakuwa na tatizo kwenye akili yako‘
‘Jana yupo mwenzetu mmoja wa kutoka Chama ninachotoka amezungumza mambo ya ajabu sana hapa, unaweza kuona ni kwanamna gani watu hawaelewi ni nani katika nyumba hii ameingia bila ya Chama kilichomleta. Wote tumezaliwa na vyama vyetu, hii michezo haitaki hasira..! ‘
‘Watu wa Dar es salaam bado wanatumia nishati ya mkaa, na Serikali inapiga vita matumizi ya mkaa. Nimwambie Waziri nguvu tunayotumia kupiga vita matumizi ya nishati hii, tutumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha tunawatafutia nishati mbadala Wananchi hawa‘
‘Tunawaambia watumie gesi hata elimu yenyewe ya matumizi ya gesi inafahamika? matumizi ya gesi hayakuanza leo, hata wasomi wenyewe wanaogopa kutumia gesi. Sasa tufanye jitihada za kutoa elimu kabla ya kuwaambia wasitumie wasitumie..!‘
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni