Dodoma, Tanzania. Mbunge wa
Bunda Mjini (Chadema), Ester
Bulaya jana alichafua hali ya
hewa bungeni baada ya kusema
kwamba Waziri wa Maliasili na
Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe ni mzigo na mwepesi
kama ‘tishu’ kwa sababu hana
uwezo wa kusimamia mambo
mazito yaliyopo katika wizara
hiyo, kama vile migogoro ya
wananchi na hifadhi za Taifa.
“Huyu waziri ni mzigo kama
alivyowahi kusema
(Abdulrahman) Kinana. Mimi
nasema yeye ni mwepesi kama
tishu, hawezi kuisaidia wizara hii
nyeti,” alisema mbunge huyo jana
wakati akichangia hotuba ya
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera,
Uratibu na Bunge, Jenista
Mhagama alisimama na kuomba
mwongozo wa mwenyekiti juu ya
mbunge huyo kutumia maneno ya
kuudhi ambao uliungwa mkono
na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew
Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta
neno mwepesi kisha aendelee na
hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya
alikataa kufuta neno hilo na
kusema wabunge hawaamuliwi
maneno ya kutumia.
Chenge aliendelea kumsihi
mbunge huyo kufuta neno hilo na
katika mabishano hayo
yaliyodumu kwa dakika tatu,
baadaye, Bulaya alikubali
kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha
neno mwepesi na kuruhusiwa
kuendelea kuchangia.
“Mwenyekiti sitafuta neno
mwepesi, kama neno ‘tishu’
linawakera basi naliondoa libaki
mwepesi,” alisema Bulaya.
Katika mchango wake, Bulaya
alisema wananchi wanaoishi
katika hifadhi zilizopo jimboni
mwake wananyanyaswa na askari
wanyamapori wakati Serikali
imeshindwa kuwatengenezea
mazingira mazuri ya kuishi.
Alimtaka waziri huyo
kushughulikia kero zote
zinazowakabili wananchi wa
Bunda akisema Serikali
haiendeshwi kwa maneno
matupu, bali vitendo na dhamira
ya dhati ya kuwahudumia
wananchi.
“Tatua matatizo jimboni kwangu
ili niweze kukupima kama wewe
ni mzito au mwepesi,” alisema
mbunge huyo akimwambia
Profesa Maghembe.
Baada ya Bulaya kumaliza muda
wake, mbunge aliyefuatia alikuwa
Abdallah Ulega wa Mkuranga
(CCM) ambaye alisema kuna haja
ya wabunge kupimwa kama
wamelewa getini ili kujua akili
zao.
“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi
kumtukana mzee kama yule
(Maghembe). Kama suala ni
uwaziri basi aangalie hata umri
wake kabla ya kuzungumza...
Naungana na aliyesema wabunge
tupimwe vilevi kabla hatujaingia
humu ndani. Unaweza kujenga
hoja yako bila kutukana, huhitaji
kutukana ili waziri atekeleze
madai yako,” alisema mbunge
huyo.
Alhamisi, 26 Mei 2016
Bulaya makubwa bungeni
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni