Ijumaa, 27 Mei 2016

Kauli ya lowasa mjini monduli

Hii ndio kauli ya mheshimiwa Lowasa kupitia ukurasa wake wap facebook baada ya kukutana na balozi wa Japan

Nimekutana na rafiki yetu Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida, nikiwa pamoja na viongozi wote wa wilaya yetu ya Monduli, mbali ya kumshukuru Balozi Yoshida kwa misaada mbalimbali wanayoitoa ila zaidi tulijadiliana jinsi gani ya kufanya muendelezo na mikakati ya kuchukulia misaada hii kama nyezo za kufikia malengo ya maendeleo na sio njia ya utegemezi kiuchumi.

Magazeti ya leo mei 28 yana sura zifuatazo

Hivi ndivyo magazeti ya Leo yalivyo

Hii ni list ya marais wa marekani tangia uhuru wake wa 1783

Jina la kwanza ni rais na la mbele ya mwaka ni la makamu wake
1 George
Washington 1789-1797 John Adams
2 John Adams 1797-1801 Thomas
Jefferson
3 Thomas
Jefferson 1801-1809
Aaron Burr
(1801-05)
George
Clinton
(1805-09)
4 James
Madison 1809-1817
George
Clinton
(1809-12)(a)
Elbridge
Gerry
(1813-14)(a)
5 James
Monroe 1817-1825 Daniel D.
Tompkins
6
John
Quincy
Adams
1825-1829 John C.
Calhoun
7 Andrew
Jackson 1829-1837
John C.
Calhoun
(1829-32)(b)
Martin Van
Buren
(1833-37)
8 Martin Van
Buren 1837-1841 Richard M.
Johnson
9 William H.
Harrison 1841 (a) John Tyler
10 John Tyler 1841-1845 vacant
11 James K.
Polk 1845-1849 George M.
Dallas
12 Zachary
Taylor
1849-1850
(a)
Millard
Fillmore
13 Millard
Fillmore 1850-1853 vacant
14 Franklin
Pierce 1853-1857 William
R.D. King
15 James
Buchanan 1857-1861 John C.
Breckinridge
16 Abraham
Lincoln
1861-1865
(a)
Hannibal
Hamlin
(1861-65)
Andrew
Johnson
(1865)
17 Andrew
Johnson 1865-1869 vacant
18 Ulysses S.
Grant 1869-1877
Schuyler
Colfax
(1869-73)
Henry
Wilson
(1873-75)(a)
19 Rutherford
B. Hayes 1877-1881 William A.
Wheeler
20 James A.
Garfield 1881 (a) Chester A.
Arthur
21 Chester A.
Arthur 1881-1885 vacant
22 Grover
Cleveland 1885-1889
Thomas A.
Hendricks
(1885)(a)
23 Benjamin
Harrison 1889-1893 Levi P.
Morton
24 Grover
Cleveland 1893-1897 Adlai E.
Stevenson
25 William
McKinley
1897-1901
(a)
Garret A.
Hobart
(1897-99)
Theodore
Roosevelt
(1901)
26 Theodore
Roosevelt 1901-1909
vacant
(1901-05)
Charles W.
Fairbanks
(1905-09)
27 William
Howard
Taft
1909-1913
James S.
Sherman
(1909-12)(a)
28 Woodrow
Wilson 1913-1921 Thomas R.
Marshall
29 Warren G.
Harding
1921-1923
(a)
Calvin
Coolidge
30 Calvin
Coolidge 1923-1929
vacant
(1923-25)
Charles G.
Dawes
(1925-29)
31 Herbert
Hoover 1929-1933 Charles
Curtis
32 Franklin D.
Roosevelt
1933-1945
(a)
John N.
Garner
(1933-41)
Henry A.
Wallace
(1941-45)
Harry S.
Truman
(1945)
33 Harry S
Truman 1945-1953
vacant
(1945-49)
Alben W.
Barkley
(1949-53)
34 Dwight D.
Eisenhower 1953-1961 Richard M.
Nixon
35 John F.
Kennedy
1961-1963
(a)
Lyndon B.
Johnson
36 Lyndon B.
Johnson 1963-1969
vacant
(1963-65)
Hubert H.
Humphrey
(1965-69)
37 Richard M.
Nixon
1969-1974
(c)
Spiro T.
Agnew
(1969-73)
Gerald R.
Ford
(1973-74)(d)
38 Gerald R.
Ford 1974-1977
Nelson A.
Rockefeller
(d)
39 James Earl
Carter 1977-1981 Walter
Mondale
40 Ronald
Reagan 1981-1989 George Bush
41 George
Bush 1989-1993 J. Danforth
Quayle
42 William J.
Clinton 1993-2001 Albert Gore
Jr.
43 George W.
Bush 2001-2009 Dick Cheney
44 Barack H.
Obama 2009- Joe Biden

Obama atua Hiroshima

Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 1939-1945 vita ya pili ya dunia ilipiganwa kwa sababu ambazo hazikumalizika wakati wa vita ya kwanza ya dunia ya mwaka 1914-1918.
Mnamo august 6 ya mwaka 1945 Bomu la atomic lilipigwa katika mji wa Hiroshima kwa makadilio liliua with 140000.
Haikua mwisho baada ya siku Tatu kupita Bomu la pili lilipigwa katika mji wap Nagasaki Bomu hili pia linakadiliwa kuua watu kati ya 70000.
Hali hii ilipelekea Japan kushindwa vita na ilipofika august 15 ya mwaka huo Japan ilijitoa rasmi kwenye vita hiyo.
Ikaliliwe kuwa tangia mwaka huo wa kumalizika kwa vita hiyo marekani chini ya Franklin Roosevelt Barack Obama ndiye rais wa kwanza wa nchi hiyo alieko madarakani kutembelea Hiroshima mbali na hivyo amezidi kuasa juu ya utumizi wa siraha za maangamizi maana no siraha zenye madhara makubwa kwa binadamu

Anusulika kifo kwa kujirusha mnarani

Kijana mmoja (pichani) jijini mwanza amenusulika kifo baada ya kujirusha kwenye mnara wa mawasiliano wa kampuni la Vodacom uliopo jirani na makutano ya barabara ya nyerere na makongolo jirani na ilipokuwa clinic.
Kijana huyo alipanda mnarani hapo majira ya saa mbili asubuhi licha ya jitihada za jeshi la zimamoto na uokoaji wakishirikiana na jeshi la polisi na raia waliokuwepo eneo la tukio kumtaka ashuke kijana huyo alizidi kupanda juu na alipo fikia kileleni mwa mnara huo aliamua kujirusha na hivi sasa yupo hospitali ya mkoa sekoutoure kwa matibabu chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Ikumbukwe kuwa kijana huyu aliwahi kupanda mnara wa sasa uliopo makutano ya makongoro na nyerere japo hakufanikiwa kutimiza azma yake

Link wazili mkuu akagua DART

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA AKAGUA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI (DART) JIJINI DAR LEO: http://othmanmichuzi.blogspot.com/2016/05/waziri-mkuu-kassim-majaliwa-akagua.html

Alhamisi, 26 Mei 2016

Bulaya makubwa bungeni

Dodoma, Tanzania. Mbunge wa
Bunda Mjini (Chadema), Ester
Bulaya jana alichafua hali ya
hewa bungeni baada ya kusema
kwamba Waziri wa Maliasili na
Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe ni mzigo na mwepesi
kama ‘tishu’ kwa sababu hana
uwezo wa kusimamia mambo
mazito yaliyopo katika wizara
hiyo, kama vile migogoro ya
wananchi na hifadhi za Taifa.
“Huyu waziri ni mzigo kama
alivyowahi kusema
(Abdulrahman) Kinana. Mimi
nasema yeye ni mwepesi kama
tishu, hawezi kuisaidia wizara hii
nyeti,” alisema mbunge huyo jana
wakati akichangia hotuba ya
Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera,
Uratibu na Bunge, Jenista
Mhagama alisimama na kuomba
mwongozo wa mwenyekiti juu ya
mbunge huyo kutumia maneno ya
kuudhi ambao uliungwa mkono
na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew
Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta
neno mwepesi kisha aendelee na
hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya
alikataa kufuta neno hilo na
kusema wabunge hawaamuliwi
maneno ya kutumia.
Chenge aliendelea kumsihi
mbunge huyo kufuta neno hilo na
katika mabishano hayo
yaliyodumu kwa dakika tatu,
baadaye, Bulaya alikubali
kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha
neno mwepesi na kuruhusiwa
kuendelea kuchangia.
“Mwenyekiti sitafuta neno
mwepesi, kama neno ‘tishu’
linawakera basi naliondoa libaki
mwepesi,” alisema Bulaya.
Katika mchango wake, Bulaya
alisema wananchi wanaoishi
katika hifadhi zilizopo jimboni
mwake wananyanyaswa na askari
wanyamapori wakati Serikali
imeshindwa kuwatengenezea
mazingira mazuri ya kuishi.
Alimtaka waziri huyo
kushughulikia kero zote
zinazowakabili wananchi wa
Bunda akisema Serikali
haiendeshwi kwa maneno
matupu, bali vitendo na dhamira
ya dhati ya kuwahudumia
wananchi.
“Tatua matatizo jimboni kwangu
ili niweze kukupima kama wewe
ni mzito au mwepesi,” alisema
mbunge huyo akimwambia
Profesa Maghembe.
Baada ya Bulaya kumaliza muda
wake, mbunge aliyefuatia alikuwa
Abdallah Ulega wa Mkuranga
(CCM) ambaye alisema kuna haja
ya wabunge kupimwa kama
wamelewa getini ili kujua akili
zao.
“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi
kumtukana mzee kama yule
(Maghembe). Kama suala ni
uwaziri basi aangalie hata umri
wake kabla ya kuzungumza...
Naungana na aliyesema wabunge
tupimwe vilevi kabla hatujaingia
humu ndani. Unaweza kujenga
hoja yako bila kutukana, huhitaji
kutukana ili waziri atekeleze
madai yako,” alisema mbunge
huyo.

Pishi la Mourinho kupakuliwa Man U

Mazungumzo baina ya meneja wa Mourinho Jorge Mendez na viongozi wa ngazi ya juu ya man u teyari yamekamilika na tangazo rasmi la klabu hiyo juu ya ujio wa kocha huyo litatolewa mapema ijumaa hii
Mourinho atachukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa Manchester Luis van Gaal msimu ulio pita

Magazeti ya kiswahili leo may 27

Hizi ni kurasa za juu za magazeti ya kiswahili

Hiki ndicho RC Makonda alichoandika kwenye ukurasa wake wa FB

Baada ya kupokea madawati hakusita kuandika haya
Asante sana MH balozi wa China Nchini Tanzania, kwanza kwakunitembelea pili kwa support ya Madawati 300 na mwisho kwa kukubali kuwa Mwenyekiti wangu wa kamati ya kuchangisha Madawati kwa Mabalozi Wote wanao Wakilisha Nchi zao hapa Tanzania

GESI bado neno zito mbunge mkuranga atoa mazito uhifadhi wa maliasili

Katika siku mbili za kujadili bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyoomba kutengewa kiasi cha Sh. 135,797,787,000 katika hotuba iliyowasilishwa na  Waziri wake Jumanne Maghembe, Wabunge walipata nafasi pia ya kuchangia ambapo hapa nakukutanisha na Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega … 

>>’Wakati mwingine hata mimi nashawishika kufikiria kwamba kabla hatujaingia kwenye jengo hili tuwe tunapimwa kama tumevuta marijuana, katika hali ya kawaida kijana hata kama umepigiwa kura na kuaminiwa na wananchi ukaenda kutukana lazima utakuwa na tatizo kwenye akili yako‘

‘Jana yupo mwenzetu mmoja wa kutoka Chama ninachotoka amezungumza mambo ya ajabu sana hapa, unaweza kuona ni kwanamna gani watu hawaelewi ni nani katika nyumba hii ameingia  bila ya Chama kilichomleta. Wote tumezaliwa na vyama vyetu, hii michezo haitaki hasira..! ‘

‘Watu wa Dar es salaam bado wanatumia nishati ya mkaa, na Serikali inapiga vita matumizi ya mkaa. Nimwambie Waziri nguvu tunayotumia kupiga vita matumizi ya nishati hii, tutumie nguvu hiyohiyo kuhakikisha tunawatafutia nishati mbadala Wananchi hawa‘

‘Tunawaambia watumie gesi hata elimu yenyewe ya matumizi ya gesi inafahamika? matumizi ya gesi hayakuanza leo, hata wasomi wenyewe wanaogopa kutumia gesi. Sasa tufanye jitihada za kutoa elimu kabla ya kuwaambia wasitumie wasitumie..!‘

Jumatano, 25 Mei 2016

Moyo mashine

Check out this blog "Usibaki nyuma hii ndio video ya ben paul.moyo mashine" http://costayego.blogspot.com/2016/05/usibaki-nyuma-hii-ndio-video-ya-ben.html

Usibaki nyuma hii ndio video ya ben paul.moyo mashine

Moyo mashine


Unaizungumziaje video hii


Ongeza afya

Kwambamji mkuu wa somalia unaitwa.......


Magazeti ya leo 26/05/2016

Hizi ni bsadhi ya kurasa za mbele za magazeti ya leo

Slaa kortin bado hapajasomeka

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam imekwama kuendelea kusikiliza ushahidi wa aliyekuwa mgombe ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) baada ya kuwekewa pingamizi na upande wa walalamikiwa, anaandika Faki Sosi.
Pingamizi hilo la kukosoa ushahidi wa Silaa limetolewa  na upande wa walalamikiwa kupitia Onesmo Kyauke, Wakili wa Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema),  mbele ya Fatuma Msengi, Jaji katika mahakama hiyo.
Wakili Kyauke amedai kuwa, hatua ya kuweka pingamizi hilo inatokana na shahidi (Silaa), kutoa ushahidi wake ambao upo nje ya kiapo.
Amesema kuwa, shahidi huyo amejibu swali wakati alipoulizwa na wakili wake ambaye ni Dk. Masumbuko Lamwai kuhusu masanduku ya kura kuchelewa kwenye baadhi ya vituo na kujibu nje ya kiapo chake, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Kutokana na sababu hiyo, Wakili Kyauke ameiomba mahakama kumzuia shahidi huyo kutoendelea na ushahidi wake pamoja na kumzuia asijibu hoja nje ya hati za kiapo.
Hata hivyo, Wakili Lamwai ameiomba mahakama kuliondoa pingamizi hilo akidai kuwa kiapo chake kinaweza kujibiwa kwa maneno na sio maandishi bila kuathiri kitu chochote.
Wakili Lamwai ametoa mfano wa rufaa ya kesi ya Zena ambayo aliieleza mahakama kuwa, atajibu kwa hati ya maandishi lakini kwenye maswali alijibu nje ya hati hiyo.
Kutokana na mvutano wa kisheria ambao uliibuka kutokana na pingamizi hilo, Jaji Msengi ameahirisha kesi hiyo hadi kesho kwa ajili ya kutoa uamuzi kuhusu ushahidi wa Silaa kuwa nje hati ya kiapo ama la.
Jana katika ushahidi wa kesi hiyo, Silaa alidai kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtishia kuchoma moto nyumba yake wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana.
Pia Silaa alidai Oktoba 27, mwaka jana katika kituo cha majumuisho ya kupigia kura cha Pugu Sekondari idadi ya wapigakura wa Chadema iliongozeka huku wakiwa wamesimama mita 20 kutokea usawa wa kituo cha majumuisho.
Silaa ambaye aliwahi kuwa Meya wa Ilala alidai kuwa, wafuasi hao walianza kuwatishia mawakala na msimamizi wa kituo jambo lililosababisha Polisi washindwe kufanya kitu zaidi ya kuwaonya pamoja na kuzungumza kihenyeji na mlalamikiwa wa pili.
“…kutokana na mazungumzo hayo, mjibu maombi wa pili na wenzake walisema hawatopokea majibu ya kupiga kura na pia watachoma moto nyumba yangu pamoja na kituo chenyewe,” alidai Silaa.

Tanzania ya viwanda yaanza kuonyesha sura yake

NDOTO ya Tanzania kuwa nchi ya
viwanda, inaelekea kutimia baada ya
Serikali ya Awamu ya Tano kuonesha
kwa vitendo dhamira yake ya
kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.
Tangu wakati wa kampeni Ilani ya CCM
ya mwaka 2015 iliponadiwa pamoja na
kauli mbalimbali za wagombea wa
chama hicho wakiongozwa na aliyekuwa
mgombea urais, Dk John Magufuli, ahadi
kubwa ilikuwa ni kujenga uchumi wa nchi
kupitia viwanda. Ahadi hiyo inatokana na
ukweli kuwa Tanzania imedhamiria
kuhakikisha ifikapo mwaka 2025,
inakuwa ni miongoni mwa nchi zilizo na
uchumi wa kati.
Katika kuhakikisha ndoto hiyo inatimia,
kupitia bajeti ya kwanza chini ya Serikali
ya Awamu ya Tano ya Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
kipaumbele kikubwa kimewekwa katika
sekta nzima ya viwanda. Hali hiyo
ilijidhihirisha tangu, Serikali ilipowasilisha
mapendekezo ya kiwango cha ukomo wa
bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha
2016/17 ambayo inaonesha kuwa
itatumika Sh trilioni 29.53 ikiwa ni
ongezeko la trilioni 7 ikilinganishwa na
bajeti ya mwaka wa fedha uliopita.
Sura hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17
inatofautiana na iliyopita iliyokuwa ya Sh
trilioni 22.45 katika maeneo mengi, ikiwa
ni pamoja na kiwango cha fedha
kitakachotengwa kwa ajili ya shughuli za
maendeleo, ambacho ni zaidi ya mara
mbili ya fedha za eneo hilo katika bajeti
iliyopita. Aidha katika mapendekezo hayo
yaliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk
Philip Mpango, shughuli zitakazopewa
kipaumbele kwenye mipango hiyo ya
maendeleo zimegawanywa katika
maeneo manne.
Maeneo hayo ni viwanda vya kukuza
uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi
wa viwanda, kufungamanisha maendeleo
ya uchumi na rasilimali watu, mazingira
wezeshi kwa uendeshaji biashara na
uwekezaji na pia usimamizi wa
utekelezaji wa mpango. Katika
kuthibitisha azma hiyo kwa vitendo,
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage,
anapowasilisha hivi karibuni bungeni
Dodoma makadirio ya mapato na
matumizi kwa mwaka wa fedha wa
2016/17 ya wizara hiyo, alibainisha wazi
kuwa kipaumbele kikubwa katika bajeti
hiyo ni kuinua sekta ya viwanda.
Anasema katika kutimiza dhana ya
Serikali ya kuijenga Tanzania yenye
uchumi wa viwanda, wizara yake
imejipanga kuhamasisha sekta binafsi
miongoni mwa Watanzania na wageni
kuwekeza kwenye sekta ya viwanda
vidogo, vya kati na vikubwa. Anasema
Serikali itawekeza nguvu zaidi kwenye
viwanda vidogo na vya kati (SMEs) kwa
kuwa ndio kwa sasa vinavyoongoza
nchini kwa kutengeneza ajira na
kuongeza pato la mtu mmoja mmoja.
Anafafanua kuwa kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na wizara hiyo, sekta ya
SMEs imetengeneza ajira takribani milioni
52 za Watanzania na kuchangia asilimia
28 kwenye Pato la Taifa (GDP). “Wizara
hii itawezesha upatikanaji wa maeneo ya
kujenga viwanda na kutoa ushauri
kuhusu upatikanaji wa mitaji na teknolojia
za kisasa. “Kwa ujumla wizara itabeba
jukumu la kuibua wana viwanda,
kuwakuza na kuwaendeleza,” anasisitiza
Mwijage.
Anaeleza kuwa kwa kuzingatia msimamo
huo, wizara hiyo itahakikisha viwanda
vilivyopo vinafanya kazi kwa uwezo
mkubwa kadri iwezekanavyo ili kudhibiti
bidhaa za nje zinazoingia nchini bila
ushindani ulio sawa. Anasema pia wizara
hiyo itaondoa vikwazo vinavyopunguza
uwezo wa kiushindani kwa viwanda
vilivyopo nchini, itahamasisha wananchi
kuwekeza katika sekta ya viwanda na
itahamasisha wawekezaji wakubwa wa
ndani na nje ya nchi kuwekeza katika
sekta hiyo.
“Nawaahidi, tutapigana kufa au kupona ili
tuwe na miundombinu wezeshi na saidizi
iliyo tayari katika maeneo ya uwekezaji
ngazi ya kanda na taifa. Nawashawishi
wazawa wanaomiliki viwanda huu ndio
wakati. Tutalinda viwanda vyenu , siwezi
kulisha mtoto wa kware, na kuacha
mtoto wa kuku afe,” anasema.
Akizungumzia maendeleo ya viwanda
nchini, Mwijage anabainisha kuwa idadi
ya viwanda nchini imeendelea
kuongezeka kutoka viwanda 125 mwaka
1961 baada ya Tanzania kupata Uhuru
hadi kufikia viwanda 49,243 mwaka
2013.
Anasema kutokana na ukweli huo
Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga
kuhakikisha inatimiza kwa kutekeleza
ahadi yake ya kuijenga Tanzania ya
viwanda kwa kuhakikisha viwanda
vinajengwa na kusambazwa nchi nzima.
Kwa mujibu wa Serikali kasi ya ukuaji wa
viwanda imekua kati ya mwaka 2006
hadi mwaka 2013 ambapo vimeongezeka
kutoka viwanda 5,153 mwaka 2005 hadi
viwanda 49,243 mwaka 2013.
Pamoja na hayo, Mwijage anabainisha
kuwa ni lengo la Serikali ya Awamu ya
Tano kuona viwanda vyote
vilivyobinafsishwa vinafanyakazi ambapo
hadi sasa ni kati ya viwanda 106
vilivyofanyiwa tathmini, 45 vinafanya kazi
vizuri, 24 vinasuasua na 37 vimefungwa.
Anasema kutokana na ongezeko hilo la
viwanda, viwanda vikubwa vinavyoajiri
kuanzia watu 100 ni 247, viwanda vya
kati vinavyoajiri kati ya watu 50 na 99 ni
170, viwanda vidogo vinavyoajiri kati ya
watu watano na 49 ni 6,907 na viwanda
vidogo sana vinavyoajiri chini ya watu
watano ni 41,919.
Anasisitiza kuwa ni lengo la Serikali ya
Awamu ya Tano kuona kuwa viwanda
vyote vilivyobinafsishwa vinafanya kazi.
“Viongozi wakuu wa nchi wamekuwa
wakisisitiza utekelezaji wa lengo hilo na
wizara yetu kwa kushirikiana na Msajili
wa Hazina tunafuatilia jukumu hilo siku
hadi siku,” anasema. Anafafanua kuwa
mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa
viwanda 37 vilivyofungwa baada ya
kubinafsishwa vinafanyiwa tathmini
haraka kabla ya nusu ya kwanza ya
mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi,
mwaka huu.
“Nasisitiza kabisa kuhusu kuwa hatma
ya viwanda visivyofanya kazi ni kwa
wamiliki waliopewa kutekeleza mikataba
ya mauzo au kupewa wawekezaji wapya
ili waviendeshe,” anasema. Aidha,
Mwijage anaeleza kuwa kupitia bajeti
hiyo na mikakati ambayo Serikali hiyo
imejiwekea, itahakikisha inahimiza na
kusimamia mpango wa viwanda sehemu
zote za nchi. Anasema tayari mamlaka
za mikoa na wilaya zimeelekezwa
kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli ya
viwanda na biashara.
“Hapa tutahakikisha kila eneo linakuwa
na kiwanda kulingana na mahitaji ya eneo
husika. Kwa mfano Tanga wanalima sana
matunda hivyo viwanda vyake vitajikita
katika eneo la kuzalisha bidhaa za
matunda kama vile juisi.” Mwijage
alisema katika kutimiza dhana ya kujenga
Tanzania yenye uchumi wa viwanda,
Wizara ya Viwanda imejipanga
kuhamasisha sekta binafsi kwa
Watanzania na wageni kuwekeza kwenye
sekta ya viwanda vidogo, vya kati na
vikubwa.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Bunge ya Viwanda na Biashara, Vicky
Kamata anapongeza hatua ya Serikali ya
Awamu ya Tano ya kuleta mapinduzi ya
viwanda na kushauri hatua madhubuti
zichukuliwe katika kushughulikia
changamoto zinazoweza kukwamisha
ndoto hiyo. “Serikali iweke kipaumbele
katika suala la kutenga ardhi kwa ajili ya
viwanda kwa kushirikisha halmashauri
za wilaya na mikoa ikiwa ni pamoja na
kujenga miundombinu bora kama vile
barabara, reli, maji, umeme na
mawasiliano,” anasisitiza

Hizi ndizo best couples zinazo zungumziwa sana Tanzania

Diamond 27 Zarina 35 difference 9 yrs.....Wolper 29 Harmonize 23 difference 7 yrs....Aunt Ezekiel 30 Mosez 23 also 7 yrs...Nisha 28 Baraka da prince 23 variation 5yrs...Shilole 29 Nedy Music 21...8 yrs....Wema Sepetu 28 Idriss 23 whch s 5 yrs... mi siwaelewi

Zambia kutumia umeme wa Tanzania

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.

Amesema  upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.

Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. 

“Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.
Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
                                                                                                     
Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable).

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

Mjusi wa lindi aibua maswali bungeni

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Mngwali amehoji Bungeni kwa nini serikali isirudishe mjusi ambaye alichukuliwa mkoani Lindi miaka ya 1900's katika kijiji cha Tandeguru kata ya Mipingo mkoani Lindi na kupelekwa ujerumani ambapo amehifadhiwa.

''Mkoa wa Lindi unaongoza kuwa na rasilimali kubwa tumepiga kelele ya mjusi, mjusi yupo ujerumani wao wanafaidika na mjusi wetu wapanata dola bilioni 3 kila mwaka sisi hatupati kitu''-Amesema Mbunge Riziki.

Mbunge huyo amebainisha kwamba kama mabaki ya mjusi huyo yangerejeshwa kwa kuwa ni kivutio kwa ukubwa wake angeweza kuhifadhiwa kwenye makumbusho nakusaidia ujenzi wa barabara na shule.

Aidha Mbunge huyo amemtaka waziri wa maliasili na utalii aeleze kwa nini tozo inayopatikana huko ujerumani haiwafaidishi wananchi wa eneo husika.

Hata hivyo mjusi huyo mara kadhaa amekuwa akiuliziwa bungeni na serikali kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kwa manufaa ya wananchi.

14 mbaroni kwa mauaji mwanza

Jeshi la Polisi Nchini linawashikilia watuhumiwa 14 kufuatia tukio la mauaji ya watu watatu lililotokea katika msikiti wa Rahman eneo la Ibanda relini mkaoni Mwanza, Mei 18 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Advera Bulimba alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Hivyo amewaomba wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili kufanikisha kuwakamata wale wote wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

“Nitoe wito kwa wananchi kushirikiana kikamilifu na vyombo vya usalama katika kufichua wahalifu kwa kuwa ni watu tunaoishi nao, hivyo hakuna budi kutoa taarifa zao ili usalama na mali zetu uendelee kuimarika”, aliongeza Kamishna Msaidizi Bulimba.

Hata hivyo, alieleza kuwa hali ya usalama nchini iko shwari na kuwatoa hofu wananchi kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwepo.

“Niwaombe wananchi kuondoa hofu juu ya hali ya usalama na wasiwasi na watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na uhalifu wanakamatwa haraka”, alisema Kamishna Msaidizi  Bulimba.

Aliongeza kuwa uchunguzi zaidi wa matukio ya uhalifu nchini unaendelea ikiwemo matukio ya mkoani Tanga, Dar es Salaam na mikoa mingine ili kubaini na kuwakamata wahusika na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Polisi zanzibar waitolea CUF uvivu

Jeshi la Polisi Zanzibar, limesema kuwa vitendo vya kihalifu vya uvunjifu wa amani vinavyotokea kisiwani Pemba vinachochewa na viongozi wakuu wa chama cha Wananchi CUF.

Akizungumza na waandishi wa habari visiwani hapa, naibu mkurugenzi wa upelelezi na Makosa ya jinai wa Jeshi hilo, Salum Msangi alisema kuwa viongozi wakuu wa CUF wamekuwa wakiwatuma wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma kisiwani Pemba kwa madai kuwa serikali iliyopo madarakani sio halali.
 
Alisema kuwa jeshi la polisi linataarifa za uhakikia kuhusu viongozi wa CUF wakiwapongeza wafuasi wao na kuwapa zawadi ya fedha kwa kuweza kufanya vitendo vya hujuma kisiwani humo ikiwemo uchomaji moto wa majengo mbalimbali na kuhujumu mikarafuu na mazao mbalimbali.
 
“Tunao ushahidi viongozi wa CUF wamewakusanya wafuasi wao na wanawapa pongezi wale ambao wameza kufanikiwa kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya wananchi”alisema.
 
Alisema kuwa jeshi hilo halitamvumilia mtu yoyote atakaehusika kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na wala halitakua na muhali katika kuchukua hatua za kisheria bila ya kujali cheo cha mtu.
 
Aidha alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia watu zaidi ya 20 kisiwani Pemba ambapo wanahusishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.
 
Akizungumzia kuhusu ripoti ya Chama cha wananchi CUF waliyoitoa juzi ya kulipeleka Jeshi hilo mahakama ya kihalifu ya kimataifa (ICC),alisema jeshi hilo haliogopi kupelekwa huko na kusema kuwa taarifa zilizomo katika ripoti hiyo zinazohusu jeshi la polisi ni za uongo.
 
“Kama ICC tutaanza kuwapeleka wao viongozi wakuu wa CUF ambao wao ndio wachochezi wakubwa wa uvunjifu wa amani ya nchi na taarifa zao zote tunazo”alisema Msangi.
 
Hata hivyo alisema jeshi la polisi linaendelea kuwaita watu mbalimbali na kuwahoji akiwemo Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.
 
Jeshi hilo liliwapa tahadhari viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa kuacha tabia ya kuwashawishi wafuasi wao kufanya vitendo vya hujuma wakati wao wametulia majumbani mwao.

Link ya Namna yanga walivyobeba ndoo ya FA

PICHA 10: Yanga walivyopokea Kombe lao la pili kwa kuifunga Azam FC Taifa http://millardayo.com/azm81ya/

Rapper young D akana utumiaji wa madawa

Young Dee amekanusha tena uvumi ulioenea mtaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds FM kinachoendeshwa na Kalapina, rapper huyo amesema tokea akiwa mdogo amekutana na mambo mengi ya kuzushiwa.

“Hata mimi nasikia sana,” alijibu alipoulizwa kuhusu tetesi za kutumia unga. “Unajua mimi nimekuwa kwenye muziki tokea niko mdogo maana tokea nipo shule nimekutana na mengi sana. Nina imani mti wenye matunda ndio hupigwa mawe, unajua sometimes wanavyosema ukifuatisha ndio unaweza kukuta kweli unaingia huko. Lakini situmii madawa ya kulevya, mimi ndio najua maisha yangu, mimi najua natumia pombe tu,” alisema Young Dee.

Alipoulizwa kwanini aliamua kuandika ujumbe kuhusu Babutale kumsaidia Chid Benz na kama hakukubaliana na Tale haya ndio yalikuwa majibu yake:

“Mimi nilihisi kitu tofauti kabisa maana Chid ni msanii mkubwa sana na haikutakiwa kumweka vile, ilitakiwa umchukue umweke sawa kimya kimya na sio vile kila mtu aone. Kama unamsaidia huo ndio ulikuwa mtazamo wangu wa tofauti, hayo mambo mengine yaliyotokea na mimi ni binadamu.”

Anna Kabwe amchunia Rc Makonda

Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkono Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.
Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.
Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.
Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Hii hapa mpya ya leo tarehe 25/05/2016

Rais JPM amteua PINDA kuwa mkuu wa chuo kikuu huria OUT

Picha bila story wolper na harmonize mahaba nikoroge

Mahaba niue