Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United
hawatakuwa wanatenda haki endapo watatoa kiasi
cha paundi mil 92 (euro mil 110) kuinasa saini ya
Paul Pogba kutoka Juventus, ada ambayo
inaelezwa kuvunja rekodi ya usajili duniani.
Scholes ni shabiki mkubwa wa Pogba lakini
amesema kwa bei hiyo inaaminisha kwamba
uwezo wake ni sawa na Lionel Messi and Cristiano
Ronaldo huku akisema haamini kwamba Mfaransa
huyo ana thamani sawa na wakali hao wawili.
“Alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa,
Nimewahi kucheza naye mara nyingi tu,” Scholes
aliwaambia wanahabari.
“Ni kweli amekuwa kwenye kiwango bora lakini
bado siamini kama ana thamani ya paundi milioni
100 kwa sasa.”
“Kwa bei kama hiyo, ungehitaji mchezaji ambaye
anaweza kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu,
kama Ronaldo au Messi, Pogba bado hajafika huko
kabisa.”
Jumamosi, 23 Julai 2016
Povu lamtoka scholes juu ya dau la pogba
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni