Ijumaa, 22 Julai 2016

Munich yajazwa damu

Watu sita wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye bunduki kuwafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani.
Polisi wanasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje.
Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, kaskazini magharibi mwa Munich.
Watu walioshuhudia tukio wanasema wamewaona watu watatu waliokuwa na bunduki.
Maafisa wa polisi Bavaria wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu Jumatatu kijana mhamiaji alipowadunga visu na kuwajeruhi watu kadha katika treni, shambulio ambalo kundi la Islamic State lilidai kuhusika.(source BBC Swahili).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni