Ijumaa, 15 Julai 2016

Ikufikie ulipo

Watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa
muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya
100 kujeruhiwa
Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo
zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma
ya kwanza vikiendelea..
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa
watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.
Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji
watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua
risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa
bomu na kufa.
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika
eneo la kuingia katika uwanja huo.
Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani
shambulio hilo na kusisitiza umoja katika
kutokomeza vitendo hivyo.
Uturuki imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya
kigaidi kutoka pande mbili,kwanza kutoka kwa
kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi jirani
ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda
dola yao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni