Paul Scholes anaamini kwamba Manchester United
hawatakuwa wanatenda haki endapo watatoa kiasi
cha paundi mil 92 (euro mil 110) kuinasa saini ya
Paul Pogba kutoka Juventus, ada ambayo
inaelezwa kuvunja rekodi ya usajili duniani.
Scholes ni shabiki mkubwa wa Pogba lakini
amesema kwa bei hiyo inaaminisha kwamba
uwezo wake ni sawa na Lionel Messi and Cristiano
Ronaldo huku akisema haamini kwamba Mfaransa
huyo ana thamani sawa na wakali hao wawili.
“Alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa,
Nimewahi kucheza naye mara nyingi tu,” Scholes
aliwaambia wanahabari.
“Ni kweli amekuwa kwenye kiwango bora lakini
bado siamini kama ana thamani ya paundi milioni
100 kwa sasa.”
“Kwa bei kama hiyo, ungehitaji mchezaji ambaye
anaweza kufunga magoli zaidi ya 50 kwa msimu,
kama Ronaldo au Messi, Pogba bado hajafika huko
kabisa.”
Jumamosi, 23 Julai 2016
Povu lamtoka scholes juu ya dau la pogba
Ijumaa, 22 Julai 2016
Munich yajazwa damu
Watu sita wanahofiwa kufariki baada ya watu wenye bunduki kuwafyatulia risasi watu katika jumba moja la kibiashara mjini Munich, Ujerumani.
Polisi wanasema washukiwa bado hawajakamatwa na wamewatahadharisha watu na kuwashauri kutotoka nje.
Operesheni kubwa ya kiusalama inaendelea katika jumba la kibiashara la Olympia, ambalo linapatikana mtaa wa Moosach, kaskazini magharibi mwa Munich.
Watu walioshuhudia tukio wanasema wamewaona watu watatu waliokuwa na bunduki.
Maafisa wa polisi Bavaria wamekuwa katika hali ya tahadhari tangu Jumatatu kijana mhamiaji alipowadunga visu na kuwajeruhi watu kadha katika treni, shambulio ambalo kundi la Islamic State lilidai kuhusika.(source BBC Swahili).
Jumanne, 19 Julai 2016
Tale kuburuzwa kortini
Mahakama imetoa hati hiyo kutokana na Babu Tale kutotii amri ya mahakama iliyomtaka amlipe Shekhe Hamis Mbonde Sh. 250 milioni.
Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
Kutokana na Babu Tale na mwenzake Iddi Tale kushindwa kulipa fedha hizo kama ilivyoamriwa tarehe 18, Februari mwaka huu, mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa wadaiwa hao tarehe 8 Julai mwaka huu.
Katika hati hiyo, mahakama ilimuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala kuwa, hadi leo tarehe 19 Julai mwaka huu awe amewakamata wadaiwa hao ili wafike mahakamani kueleza kwanini wasipewe adhabu kwa kukiuka amri ya mahakama.
Shauri hilo limetajwa tena leo mbele ya Juma Hassan, Kaimu Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ambapo ametoa hati nyingine kumuelekeza Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni kuwakamata wadaiwa hao.
Msajili Juma ametoa hati hiyo baada ya Mwesigwa Muhingo, Wakili wa Shekhe Mbonde, kuomba hati hiyo ipekwe Kinondoni kwa kuwa Babu Tale anaishi huko na si Wilaya ya Ilala kama hali ya kwanza ilivyoeleza.
Tarehe 18 Februari mwaka huu, Jaji Augustine Shangwa, aliwaamuru wadaiwa kulipa Sh. 200 milioni kama fidia ya kuvunja haki miliki ya Shekhe Mbonde na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunja makubaliano.
Katika uamuzi wake Jaji Shangwa amesema, Juni 16, 2013, Mbonde aliingia makubaliano na wadaiwa hao na wenzake ya kufanya biashara ya kurekodi mawaidha na kutengeneza nakala DVDs kwa ajili ya kuziuza nchini.
Wadaiwa hao waliahidi kumjengea nyumba, kumnunulia gari na kuitangaza kazi yake pia walimpa Sh milioni mbili na kumnunulia kanzu na kofia (baraghashia) na kurekodi DVDs zenye ujumbe Uzito wa Kifo, Fitina Juu ya Wanawake, Umuhimu wa Swala, Mwanadamu Yumo Ndani ya Hasara na Maadui wa Uislam.
Amesema, makubaliano ya awali yalikuwa kurekodi halafu baadaye wakubaliane kuhusu bei na jinsi ya kuziuza, badala yake waliziuza na kuzisambaza nakala hizo na kujipatia faida bila kumshirikisha Mbonde ambaye alitumia ujuzi wake.
Mbonde kupitia wakili wake Muhingo, Gwamaka Mwaikugile na Clement Kihoko, alifungua kesi ya madai namba 185/2013 akiiomba mahakama iamuru wadaiwa wamlipe Sh. 700 milioni kama fidia ya kuvunja makubaliano na Sh. 50 milioni kama fidia ya hasara aliyoipata kutokana na kuvunjwa kwa makubaliano
Jumapili, 17 Julai 2016
Zawadi za rigi kuu msimu uliopita teyari ziko hewani
Hitimisho ligi ya msimu wa 2015/2016 imekamilika kwa utolewaji wa zawadi kwa washindi wa kombe la msimu wa 2015/2016 ulioambatana na utoaji wa tuzo kwa vipengele mbalimbali.
Mgeni rasmi katika halfa hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Mwigulu Nchemba amemtaja mchezaji bora wa msimu kuwa ni Juma Abdul wa Yanga ambaye amewashinda wenzake ambao ni Mohammed Hussein na Chiza Kichuya.
Juma Abdul kwa msimu umeomalizika amecheza michezo 25, dakika 2,069 na kufanikiwa kufunga magoli 3 huku akipewa kadi moja ya njano.
Orodha kamili ni;
Mchezaji Bora wa Msimu – Juma Abdul – Milioni 9.2
Mchezaji Bora Chipukizi – Mohammed Hussein – Milioni 4
Mchezaji Bora wa Kigeni – Thaban Kamusoko – Milioni 5.7
Goli Bora la Msimu – Ibrahim Ajib – Milioni 3
Golikipa Bora wa Msimu – Aishi Manula – Milioni 5.9
Kocha Bora wa Msimu – Hans Van Der Pruijm – Milioni 8
Refa Bora wa Msimu – Ngole Mwangole
Timu Yenye Nidhamu – Mtibwa Sugar – Milioni 17.2
Mfungaji Bora Msimu wa 2015/2016 – Amissi Tambwe – Milioni 5.7
Washindi wa msimu;
4. Prisons – Milioni 21
3. Simba – Milioni 29
2. Azam – Milioni 42
1. Yanga – Milioni 81
Ijumaa, 15 Julai 2016
Ikufikie ulipo
Watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa
muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Ataturk Istanbul nchini Uturuki,na wengine zaidi ya
100 kujeruhiwa
Shughuli za usafirishaji katika uwanja huo
zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma
ya kwanza vikiendelea..
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa
watu hao 32 na idadi hiyo ya majeruhi.
Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji
watatu,ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua
risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa
bomu na kufa.
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika
eneo la kuingia katika uwanja huo.
Rais wa Uturuk Recep Tayyip Erdogan amelaani
shambulio hilo na kusisitiza umoja katika
kutokomeza vitendo hivyo.
Uturuki imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi ya
kigaidi kutoka pande mbili,kwanza kutoka kwa
kundi la Islamic State wanaoingia kutoka nchi jirani
ya Syria na waasi wa Kikurud wanataka kuunda
dola yao.
Mapinduzi uturuki
Kundi moja la kijeshi nchini Uturuki linasema
limechukua udhibiti wa nchi huku milio ya risasi
ikisikika jijini Ankara
15 Julai 2016
36 teyari wameripotiwa kuuwawa
Obama atuma salamu
SAMATTA atia mchango wake
usiku Juni 14, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta alifunga goli kwenye mchezo wa hatua za awali kuwania kucheza Europa Ligue wakati Genk ikicheza dhidi ya Buducnost Podgorica.
Mchezo huo ulimalizika kwa Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 huku Samatta akiwa amefunga bao la pili dakika ya 79 huku baada ya Neeskens Kebano kufunga bao la kwanza dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati.
Alhamisi, 14 Julai 2016
Zitto na ukapela basi
Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi wa ACT tarehe 14/07/2016 afunga ndoa huko Zanzibar na kuuanga ukapela rasmi chini ni picha za tukio hilo